Tuesday, June 13, 2017

Maoni ya Tundu Lissu baada ya Rais Magufuli kupokea ripoti ya pili ya kamati maalum ya uchunguzi wa madini


For the Record: What Goes Around Comes Around!!!

Leo wapinzani wa Serikali ya Magufuli tumesemwa sana na kutishiwa kushughulikiwa bungeni na nje ya Bunge.

Kwa sababu hiyo, naomba niweke rekodi ya masuala haya sawa sawa.

Mwezi Machi '97 Bunge lilipitisha Sheria 2 kwa siku moja kwa kutumia Hati ya Dharura.

1) Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbali mbali za Fedha ya '97 ilifuta au kupunguza kodi nyingi kwa ajili ya makampuni ya kigeni ya madini.

2) Sheria ya Uwekezaji Tanzania '97 iliwapa wawekezaji wa kigeni ulinzi mkubwa na manufaa mengi kama vile kuondosha nje fedha na faida yote wanayopata kwa uwekezaji wao nchini.

Mwaka '98 Bunge lilipitisha Sheria ya Madini '98 ambayo ilitamka kwamba mwenye milki ya madini na fedha yote itokanayo na mauzo ya madini ni mwenye leseni ya kuchimba madini hayo.

Sheria hizo tatu nimeziita 'Utatu Usio Mtakatifu' (Unholy Trinity) katika maandiko yangu mbali mbali, na nimezichambua sana tangu mwaka '99 nilipoanza harakati dhidi ya sekta ya madini ya aina hii.

Kwa miaka yote hii hadi leo, Sheria hizi za madini zimeungwa mkono na kupigiwa debe na kila kiongozi na mbunge wa CCM, Magufuli included.

Watu hawa, with very few and minor exceptions, ndio wamekuwa washangiliaji wakubwa wa unyonyaji wa makampuni ya kigeni ya madini katika nchi yetu.

Na ukweli ni kwamba watu hawa na Chama chao ndio wamefaidika sana na utaratibu huu katika sekta ya madini.

Wachache tuliopinga utaratibu huu tuliitwa kila aina ya majina mabaya na uzalendo wetu ulihojiwa kama unavyohojiwa leo na Magufuli.

Kwa mfano, Rais Mkapa alidai, wakati anazindua Mgodi wa Bulyanhulu, kwamba upinzani wetu ulikuwa ni 'ujinga uliofichama katika kivuli cha taaluma.'

Baadhi yetu, kama mimi na Dr. Rugemeleza Nshala, tulikamatwa na kushitakiwa mahakamani kwa uchochezi. Tulikabiliwa na kesi hiyo kuanzia Mei '01 hadi '08 ilipofutwa kwa kukosekana ushahidi.

Kama ilivyokuwa wakati wa Mkapa mwaka '01, leo pia Rais Magufuli ametukebehi na kuahidi kutushughulikia 'tukiropoka' nje ya Bunge.

Tunaambiwa ni lazima tumuunge mkono Rais wetu katika hii 'vita ya uchumi.' Ni sheria ipi ya Tanzania inayotulazimu kumuunga mkono Rais wetu hata kama tunaona amekosea???

Hebu naomba tuitafakari hii 'vita ya uchumi' kidogo. Je, nani hasa ni maadui zetu katika 'vita' hii??? Ni makampuni ya madini ya kigeni??? Kama ni hivyo, fikiria yafuatayo:

1) Wakati tuko vitani, Rais Magufuli na serikali yake wameiruhusu Acacia Mining (tunayoambiwa hata haijasajiliwa!!!) kuendelea kuchimba, kusafisha na kusafirisha nje ya nchi dhahabu kutoka Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara Tarime.

Amezuia magwangala yasisafirishwe nje kwenye makontena lakini dhahabu yenyewe hamna shida ikisafirishwa na wezi hawa!!!!!

2) Wakati mapambano ya 'vita ya uchumi' yakiendelea, dhahabu yote inayochimbwa Geita Gold Mine (Mgodi mkubwa kuliko yote nchini) inaendelea kuchimbwa, kusafishwa na kusafirishwa nje ya nchi.

3) Wakati tuko vitani, Rais Magufuli na serikali yake ameruhusu kila mgodi wa dhahabu nchini kuwa na kiwanja chake binafsi cha ndege ili wezi hawa waweze kutorosha 'dhahabu yetu' kwa urahisi zaidi.

4) Wakati tungali vitani, 'Utatu Usio Mtakatifu' wa sheria zetu za kodi, uwekezaji na madini uko pale pale ulipokuwa mwaka '97-'98, cosmetic changes excepted.

Aidha, licha ya kuwa vitani, sisi bado ni signatories wa MIGA Convention na bilateral investment treaties (BITs) zinazowalinda hawa tunaoaminishwa kuwa ni wezi na maswahiba wao wa miaka yote.

5) Wakati tuko kwenye hii vita kubwa ya uchumi, jemedari wetu mkuu na serikali yake hawajatengua mkataba hata mmoja wa uendelezaji madini (Mineral Development Agreements - MDAs) walizosaini hawa anaowaita wanyonyaji na serikali za watangulizi wake Jakaya Kikwete na Ben Mkapa.

6) Wakati tunahamasishwa kumuunga mkono jemedari huyu shupavu, bado hatujaonyeshwa mkataba hata mmoja waliosaini na wanyonyaji hawa tangu miaka ya mwanzo ya '90.

Leo Jemedari Mkuu ameahidi kwamba mikataba hiyo italetwa bungeni. Safi sana.

Lakini je, hii ni mara ya kwa

No comments:

Post a Comment